Ilikuwa 2021 nakumbuka ilikuwa mwezi wa 4, humu Facebook nilikutana na binti mrembo hivi, yeye ndo a... - AI Avatar by DASTAN MWAKAPEJE | Percify AI Avatar Generator

Ilikuwa 2021 nakumbuka ilikuwa mwezi wa 4, humu Facebook nilikutana na binti mrembo hivi, yeye ndo alianza kuniomba urafiki, nilimkubalia ikawa ni mwendo wa Kila mmoja akipost tuna komentiana na kulike, ilipita mwezi mzima hakuna aliye mtafuta mwenzie inbox. Siku Moja nikiwa online usiku saa sita, yeye ndo alinitumia ujumbe inbox, " wewe mtu hulali tu"? Na Mimi nikamwuliza "mbona wewe hujalala" akasema Hana usingizi, tulichat kidogo nikawa nimelala, kesho yake asubuhi akanitumia ujumbe inbox "umeamkaje" nikamjibu salama, hapo hapo akanitumia namba yake ya simu bila kumuomba, akaniambia hiyo namba chukua tutakuwa tuna juliana hali, nikasema sawa. Baada ya wiki tulijikuta tuna ingia kwenye mahusiano rasmi, alikuwa binti mrembo wa kisukuma, anavaa nguo za kujistiri sana, Yani Kwa kifupi alionekana ni binti ambaye kalelewa katika maadili ya kikristo hata katika uongeaji wake, Kila jumapili anakuambia anaenda kanisani, ijumaa kwenye maombi, hayo tu yalitosha kuamini nimepata mke na nikawa Niko tayari Kwa Kila kitu, akili yangu ikaanza kufikiria tu kuhusu ndoa kitu ambacho mwanzoni sikuwahi kufikiria. Mwezi wa sita mwaka huo 2021 aliniomba aje kwangu Ili tuonane, nikasema haina shida, nikamtumia laki na nusu, afanyie maandalizi na nauli pia, Yani nilituma hiyo pesa nikiwa Sina shaka juu yake, Nakumbuka pesa nilimtumia kama ijumaa huku safari ilitakiwa aanze jumatatu, siku hiyo ya jumatatu niliamka nikiwa na furaha kwamba usiku naenda nampokea kipenzi changu, Lakini ilivyo fika saa mbili asubuhi nikawa napiga simu haipatikani, nikawa najipa matumaini kuwa labda Huenda ni mtandao njiani, nikawa napiga namba zake zote mbili hazipatikani, bado nikawa najipa matumaini ni mtandao. Saa tano asubuhi, nilipiga tena simu ikaita lakini haikupokelewa, piga tena, simu haipokelewi, mpaka saa kumi jioni simu haipokelewi, na mwisho kabisa akaniblock Kila sehemu, namba unayo piga inatumika, Facebook pia nikawa nimesha blokiwa. Pale pale nikasema tayari nime tapeliwa, na Wala sikujaribu kumtafuta Kwa namba nyingine, ilibidi tu nimwachie MUNGU, ila ukweli ni kwamba niliumia sana, sijawahi kupata maumivu kama Yale aliyo nifanyia yule binti, nililia usiku Kwa uchungu mno. 2023 mwezi wa Saba nikiwa kazini asubuhi nilipigiwa simu na namba ngeni, nilivyo pokea, nikasikia sauti ya kike ambayo haikuwa ngeni masikioni mwangu akiwa anaongea Kwa hofu, alianza na neno samahani, akajitambulisha jina lake, Kweli niliye mfikiria alikuwa ni yeye, akasema, yeye Yuko muhimbili ame muuguza mama yake alivunjika nyonga, Wana siku tatu wako pale, binti akasema yeye analala nje pale hospital, ndugu waliye mtegem@ea hajaja hata kuwaona, nilicho mjibu nilimwambia jioni nikitoka kazini nitapitia hospital kuwaona. Jioni saa 11 nilifika pale muhimbili nikampigia simu anielekeze ni wodi Namba ngapi, akaniambia nikae Getini anakuja kunifuata, nikasema sawa. Nilimsubiri pale Getini, mara simu ikapigwa akaniuliza uko wapi? Nikamwambia zilipo paki Bajaj, nilimuona binti mrembo Asiye na mambo mengi Akija anaongea na simu nikajua ndo yeye, nikamfuata, tukasalimia japo alikuwa na aibu sana iliyo changanyika na hofu lakini nikawa namuonyesha uso wa tabasamu ila moyoni roho imefunga vibaya Kwa hasira. Tulienda mpaka wodini, nilimkuta kweli mama yake kalala kitandani kawekewa chuma, nilimsalimia yule mama, alionekana ni mtu wa Imani sana mana biblia ilikuwa Iko pembeni ya kichwa chake, nilipiga sana stori na mama huku binti kakaa pembeni anatusikiliza tu huku ananitazama Kwa kuibia. Muda wa kuona wagonjwa uliisha nikawa nime wakabidhi vitu nilivyo wanunulia, nikawaambia Kila jioni nitakuwa naenda kuwaona, yule mama alifurahi sana na akawa ameshusha maombi kwangu, alivyo maliza nikawaaga Ili niondoke, yule mama akaniomba niende na binti yake mana Hana pakulala,analala nje na Kuna mbu hatari, nilijifikiria sana, nikawaza sana, Sasa nikajisemea kwangu naishi mwenyewe na nimepanga chumba na sebule itakuwaje?! Nikisema nimpeleke kwetu awe analala huko napo ni mbali na muhimbili ilipo, nikasema potelea mbali acha niende naye nitamwachia chumba nitakuwa nalala sebuleni. ITAENDELEA Kama utapenda hii iendelee naomba weka comment na like, pia share Kwa wingi. Dastan Qsa TZ @highlight #viralreelschallenge2025viralreelschallengejaiviralreelschallengeviralreelschallenge

28

Views

0

Likes

0

Comments

0

Shares

#people#storytelling
Oct 23, 2025
photo

Comments (0)